LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wasafiri katika kivuko cha Kisorya Bunda waanza kupimwa joto la mwili

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI, limekabidhi mashine ya kupima joto la mwili (Thermometer) katika kivuko cha Kisorya kinachounganisha Wilaya ya Bunda mkoani Mara pamoja na Ukerewe mkoani Mwanza.

Akizungumza Jumatano Aprili 29, 2020 wakati wa kukabidhi mashine hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Yassin Ally aliwahimiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona hususani kuhakikisha watoto hawazururi mitaani wakati huu shule zimefungwa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwahimiza wanajamii kutojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kuwaoza wanafunzi wa kike kwa kuwadanganya shule zimefutwa kutokana na janga la Corona.
 Mkuu wa Wilaya Bunda mkoani Mara, Lidya Bupilipili (kushoto) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bunda, Kelvin Ochieng (kulia) mashine ya kupima joto la mwili (Thermometer) iliyotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ajili ya kutoa huduma katika kivuko cha Kisorya.
 Mkuu wa Wilaya Bunda mkoani Mara, Lidya Bupilipili (kulia) akizindua zoezi la upimaji joto la mwili kwa wasafiri wa kivuko cha Kisorya baada ya Shirika la KIVULINI kukabidhi mashine ya 'Thermometer' kivukoni hapo.
 Mkuu wa Wilaya Bunda mkoani Mara, Lidya Bupilipili (kulia) akizindua zoezi la upimaji joto la mwili kwa wasafiri wa kivuko cha Kisorya .
Mkuu wa Wilaya Bunda mkoani Mara, Lidya Bupilipili (kulia) akizindua zoezi la upimaji joto la mwili kwa wasafiri wa kivuko cha Kisorya baada ya Shirika la KIVULINI kukabidhi mashine ya 'Thermometer' kivukoni hapo.
Mkuu wa Wilaya Bunda, Lidya Bupilipili akinawa mikono kabla ya kuingia katika kivuko cha Kisorya wilayani humo. 
 Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akinawa mikono kabla ya kuingia katika kivuko cha Kisorya wilayani Bunda.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.