LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Magu ahimiza wananchi kuendelea kujifukiza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Mkuu wa Wilaya Magu mkoani Mwanza, Dkt. Philmon Sengati amewahimiza wananchi kuendelea kuzingatia tahadhari za kujikinga na maambukizi dhidi ya virusi vya Corona (Covid- 19) ikiwemo kutumia njia za asili za kujifukiza kama ilivyoshauriwa na Rais Dkt. John Magufuli.

Dkt. Sengati ameyasema hayo Jumatano Aprili 29, 2020 wakati akipokea mashine tano za kupima joto la mwili pamoja na vitakasa mikono lita 10 zilizoolewa na Shirika la KIVULINI ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na Corona.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Shirika la KIVULINI limekabidhi vifaa vya kusaidia mapambano dhidi ya Corona katika Wilaya Magu vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.8 (Tsh. Milioni 1,840,000).
 Wafanyabiashara wa soko kuu mjini Magu wakipima joto la mwili baada ya kupokea kifaa cha huduma hiyo kutoka Shirika la KIVULINI.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.