LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwanza "Shirika la Kivulini lakabidhi mashine za kupima joto"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI limekabidhi vifaa vya kupimia joto pamoja na dawa za kutakasa mikono ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid- 19).

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Yassin Ally amekabidhi vifaa hivyo Jumanne Aprili 28, 2020 kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kwa ajili ya kuvigawa katika taasisi mbalimbali hususani zinazohudumia idadi kubwa ya wanawake ikiwemo dawati la jinsia la polisi.

Shirika la KIVULINI limesaidia upatikanaji wa vitakasa mikono pamoja na mashine 18 za kupima joto zenye thamani ya shilingi milioni 6.3 ambazo zitapekekwa katika maeneo mbalimbali ya umma ili kusaidia mapambano dhidi ya Corona.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) mashine za kupima joto.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa dawa ya kutakasia mikono (sanitizer) iliyotolewa na Shirika la KIVULINI.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa dawa ya kutakasia mikono (sanitizer) iliyotolewa na Shirika la KIVULINI kwa ajili ya jeshi la polisi.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikabidhi mashine ya kupima joto kwa jeshi la polisi.
 Shirika la KIVULINI limesaidia upatikanaji wa mashine 18 za kupima joto zitakazopelekwa katika maeneo mbalimbali yenye msongamano wa watu.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.