LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tanzania yaporomoka tena viwango vya Uhuru wa Habari Duniani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Yohan Gwangway, Mwanza
Ikiwa leo ni siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani, taifa la Tanzania linaendelea kuporomoka katika viwango vya kulinda Uhuru wa waaandishi wa habari duniani. 

Katika ripoti ya waaandishi wasio na mipaka( Reporters Without Borders) ya Mwaka 2020 Tanzania imeshuka kwa nafasi 6 kutoka nafasi ya 118 Mwaka uliopita hadi nafasi ya 124 kwa Mwaka huu kati ya nchi 180.

Kwa maana hii basi Tanzania imeshuka kwa nafasi 53 kutoka mwaka 2016 hadi mwaka huu kwani mwaka 2016 Tanzania ilikuwa nchi ya 71 katika viwango vya kulinda Uhuru wa vyombo vya habari. Kutoka nafasi ya 71 hadi ya 24 ndio taswira ya hali yetu katika Uhuru wa vyombo vya habari.

Hii ni namna Tanzania ilivyoporomoka;
2016 nafasi ya 71
2017 nafasi ya 83
2018 nafasi ya 93
2019 nafasi ya 118 
2020 nafasi ya 124 

Ukifanya mlinganisho na majirani zetu Kenya ambao mwaka 2016 wao walikuwa nafasi ya 100 ni kuwa nchi hiyo imeendelea kuwa juu ya Tanzania kwa viwango vya Uhuru wa vyombo vya habari. 

Hizi ni nafsi za Kenya tangu mwaka 2016;
2016 nafasi ya 100
2017 nafasi ya 95
2018 nafasi ya 95
2019 nafasi ya 96
2020 nafasi ya 100

Kwa maana hii ukifanya mlinganisho wa nchi hizi mbili kwa miaka 5 Yaani mwaka 2016 hadi 2020 ni kuwa Kenya haijashuka hata nafasi moja wakati Tanzania ikiporomoka kwa nafasi 53 ndani ya miaka 5. Kenya imesalia katika nafasi ya 100 ya mwaka 2016 licha ya kupanda katika miaka hapa katikati.

Sababu mbalimbali zinaendelea kutajwa kwa mporomoko huu wa Tanzania ikiwa ni pamoja na baadhi ya sheria, fungiafungia ya vyombo vya habari, kukamatwa kwa waaandishi, kupotea kwa waaandishi ( Azory Gwanda) na mazingira ya utendaji kazi wa waaandishi hapa nchini.

Kwa eneo la Afrika mashariki Burundi inaburuza mkia ikiwa nafasi ya 159, Rwanda nafasi ya 155, Sudan kusini 139 na Uganda ikiifuata Tanzania kwa kushika nafasi ya 125.

Kwa mujibu wa ripoti hii nchi ya Turkmenistan ndio sehemu hatari zaidi duniani kufanya kazi ya uandishi wa habari ikishika nafasi ya 180 kati ya nchi 180 zilizopo katika ripoti hii. Taifa la Norway lenyewe limeendelea kushika nafasi ya 1 kwa mwaka wa 3 mtawalia.

Ripoti hii inataja nchi ya Namibia kuwa katika nafasi ya kwanza Afrika na ya 23 duniani kwa kujali Uhuru wa vyombo vya habari. Hizi ni nchi 5 zilizoshika nafasi ya juu katika ripoti ya hii kwa mwaka 2020

Tano bora Afrika;
1: Nambia ya 23 duniani
2: cape Verde ya 25 duniani
3: Ghana ya 27 duniani
4: Afrika kusini ya 31 duniani
5: Burkinafaso ya 36 duniani

MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI 2020.
Ndugu wanachama, leo Mei 3, 2020 kimsingi ni siku pekee Duniani, ambapo waandishi wa habari wote Duniani tunaadhimisha maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " UANDISHI WA HABARI USIO NA MASHAKA WALA UPENDELEO"

Ndugu wanachama maadhimisho ya mwaka huu yamekuwa ni tofauti kidogo na miaka ya nyuma, hii ni kutokana na kuibuka kwa janga la ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Kwa mwaka huu 2020 siku ya leo wanahabari kote Duniani tunaadhimisha kwa njia tofauti na miaka ya nyuma, kwa  mwaka huu waandishi tunashiriki tukiwa tumejifungia Majumbani na wengine wakishiriki maadhimisho hayo kwa njia ya teknolojia ya mitandao.

Ndugu wanachama  licha ya janga hili la corona bado dhima ya vyombo vya habari ipo pale pale ikiwa ni kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii. Mambo haya yote yanachagizwa na kusema ukweli. Dhima kuu ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari kila mwaka ni kuwakumbusha wenzetu ambao walipata madhira wakiwa wanatekeleza kazi zao.

Pia kujadili changamoto zinazotukabili na kuja na suluhisho la namna ya kuyakabili.
Ndugu wanachama kwenye maadhimisho ya mwaka huu, tumeshuhudia Nchi yetu (Tanzania) ikiwa imeporomoka kwa nafasi sita kwenye kuheshimu uhuru wa habari kwa mujibu wa ripoti ya Waandishi wa habari wasio na mipaka, kwa mwaka 2019 tulishika nafasi ya 118 na mwaka huu 2020 tuneshika nafasi ya 124.

Ndugu wanachama, ni wazi kuwa waandishi wa habari wanafanya kazi kwenye mazingira magumu ikiwemo , kufanya kazi bila mikataba, malipo duni, masaa mengi ya kazi yasiyo na malipo, mazingira ya kazi yasiyo rafiki, sheria kandamizi, hofu, uhaba wa vitendea kazi, ukosefu wa bima za kazi na mengineyo.

Hizi zote ni changamoto kubwa kwetu, ambazo zinarudisha nyuma wajibu wa mwandishi hapa Nchini.  Nini tufanye? kila mmoja kwa nafasi yake anawajibika kuhakikisha anazishinda changamoto hizi. Wajibu wa taasisi yetu na nyinginezo ni kuhakikisha tunatafuta majibu ndani ya changamoto hizi na kufanya taaluma ya habari isonge mbele.

Ndugu waandishi tunajua kuwa, tumekosa fursa ya kukutana kwa pamoja ili tuongee ana kwa ana na kutoa dukuduku zetu, haya yote yasitufanye tutengeneze ukuta wa kujadili matatizo yetu, tue delee kutumia teknolojia kuwasiliana na kubadilishana uzoefu wetu.

 Usamala wetu,  Ndugu wanachama usalama wetu ni muhimu sana, tuhakikishe tunapofanya kazi zetu tunakuwa salama, usalama wa kwanza unaanzia kwa mwandishi mwenyewe.
 Taasisi itahakikisha pia inawalinda wanachama wake wote, kwa kuwa usalama ndio hazina ya kwanza ya wanachama. Nawaomba tutekeleze wajibu wetu bila mashaka wala upendeleo kama kauli mbiu yetu ya mwaka huu inavyosema.

 Ahsanteni
Nawatakia maadhimisho mema ya vyombo vya habari kwa mwaka 2020
Edwin Soko, Mwenyekiti Mwanza Press Club.

No comments:

Powered by Blogger.