LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la WoteSawa lakabidhi vifaa kwa wafanyakazi wa nyumbani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani (WoteSawa) Jumamosi Mei 23, 2020 limekabidhi vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19) kwa wanawake wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Angel Benedicto amesema vifaa hivyo ikiwemo sabuni, barakoa pamoja na vitakasa mikono vitawasaidia wanawake hao kujikinga na kuwakinga wengine na maambukizi ya Corona wakati wakitimiza majukumu yao.
#BMGHabari 
 Mkurugenzi wa shirika la WoteSawa, Angel Benedicto akigawa vifaa vya kujikinga na Corona kwa wanawake wanaofanya kazi za kutwa majumbani.
Mkurugenzi wa shirika la WoteSawa, Angel Benedicto (kulia) akiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.