LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wazazi waonywa kuwaoza watoto wa kike “wanadanganya wamepotea”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Baadhi ya wazazi wilayani Bunda wametakiwa kuacha tabia ya kuwaoza watoto wao wa kike huku wakiripoti polisi kwamba wamepotea. Visa vya aina hiyo vimetajwa kuibuka katika kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kutokana na janga la Corona.

Hayo yalielezwa Aprili 30, 2020 wakati wa zoezi la kukabidhi mashine ya kupimia joto la mwili (Thermometer), vitakasa mikono (sanitizer) pamoja na fedha shilingi laki tano vilivyotolewa na shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana KIVULINI kwa jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia wilayani Bunda.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Wilaya Bunda, Lidya Bupilipili (kulia) akimkabidhi mashine ya kupima joto la mwili Mkuu wa Polisi Wilaya Bunda, Athuman Mkulindi (kushoto). Mahine hiyo imetolewa na shirika la KIVULINI.
 Mkuu wa Wilaya Bunda, Lidya Bupilipili (kushoto) akikabidhi vitakasa mikono lita tano kwa jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya Bunda, Lidya Bupilipili (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Polisi Wilaya Bunda fedha shilingi laki tano (Tsh. 500,000) zilizotolewa na shirika la KIVULINI kwa ajili ya kusaidia doria ya kupambana na ukatili wa kijinsia.
 Mkuu wa Wilaya Bunda, Lidya Bupilipili (kushoto) akimpima joto la mwili Mkuu wa Dawati la Jinsia la Polisi wilayani Bunda.
 Mkuu wa Wilaya Bunda, Lidya Bupilipili (kushoto) akimpima joto la mwili mmoja wa akina mama wilayani humo kupitia mashine ya kupima joto la mwili iliyotolewa na shirika la KIVULINI kwa jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.