LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA “UWT wakabidhi vifaa vya kujikinga na Corona”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa Mwanza imempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna alivyoliongoza vyema Taifa kwenye mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Hellen Bogohe ametoa pongezi hiyo Juni 08, 2020 wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella vifaa vya kusaidia mapambano dhidi ya Corona ikiwemo ndoo, sabuni pamoja na barakoa.


“Corona imepungua lakini bado tunatakiwa tuendelee kujikinga” amesisitiza Bogohe huku akimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake ikiwemo kuliongoza Taifa kwenye maombi wakati wa mapambano dhidi ya virusi hivyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kulia) akipokea vifaa vya kusaidia mapambano dhidi ya Corona kutoka kwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa Mwanza, Hellen Bogohe (wa pili kushoto).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amesema vifaa hivyo vitasaida kutoa huduma katika maeneo yenye uhitaji ikiwemo mashuleni pamoja na maeneo ya kutolea huduma za afya.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akipokea barakoa kutoka kwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa Mwanza, Hellen Bogohe (wa pili kushoto).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) akipokea vifaa vya kusaidia mapambano dhidi ya Corona kutoka Jumuiya ya UWT Mkoa Mwanza.
Viongozi mbalimbali wa UWT Mkoa Mwanza wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Hellen Bogohe (kulia).
Viongozi wa UWT Mkoa Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.