LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko ashuhudia STAMICO ikisaini mkataba mnono GGM

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameshuhudia Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) likisaini mkataba wa kuchoronga miamba katika mgodi wa dhahabu Geita (GGML) wenye thamani ya shilingi Bilioni 5.6 katika kipindi cha miezi sita.


Hafla ya utiaji saini mkatana huo imefanyika Jumatano Julai 22, 2020 mjini Geita na hivyo kufungua fursa mpya kwa Shirika la STAMICO lililoanzishwa mwaka 1972 kushiriki katika kandarasi mbalimbali ikiwa ni jitihada za kuhakikisha linajiendesha kwa faida tofauti na ilivyokuwa hapo awali kabla ya mabadiliko ya kiuongozi yaliyofanyika hivi karibuni.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo ameitaka STAMICO kutekeleza vyema kandarasi hiyo ili kufungua fursa zaidi kwa watanzania kushinda kandarasi katika migodi mbalimbali.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amesema Serikali itahakikisha shirika la STAMICO linajiimarisha na kujiendesha kwa faida tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Venance Bahati ameahidi kusimamia utekelezaji wa maagizo mbalimbali yaliyotolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko ikiwemo kutekeleza vyema na kwa wakati kandarasi ya uchorongaji miamba katika mgodi wa GGML.
 Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amehimiza STAMICO kuwatumia watanzania kwenye utekelezaji wa kandarasi hiyo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa mgodi wa GGML, Richard Jordinson (kulia) akikabidhiana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Venance Bahati (kushoto).
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.