LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Lukuvi aagiza Ofisi za Ardhi kuacha urasimu “zitatue migogoro”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameziagiza Ofisi za Ardhi katika mikoa yote nchini kuhakikisha hadi kufikia Disemba 30, 2020 ziwe zimetatua migogoro mbalimbali ardhi ikiwemo mipaka pamoja na fidia kwa wananchi.

Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo Jumatatu Julai 06, 2020 wakati akizindua Ofisi ya Ardhi Mkoa Geita na kuongeza kuwa ofisi hizo zinapaswa kuondoa urasimu na kushughulikia kwa wakati changamoto za wananchi hususani upatikanaji wa hati ndani ya siku saba baada ya kusaidia.

"Kila mkoa lazima uwe na kitabu kinachoorodhesha migogoro ya ardhi na ratiba ya namna ya kutatua migogoro hiyo. Mpaka tarehe 30 mwezi Disemba mwaka huu nisisikie tena kuna migogoro ya ardhi" amesisitiza Waziri Lukuvi huku akiwataka Watendaji kuwasaidia Wakuu wa Wilaya na Mikoa utaalamu wa kutatua migogoro hiyo.

Awali Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa pongezi kwa Waziri Lukuvi kwa namna Wizara yake inavyojitahidi kutatua migogoro ya ardhi na kumuomba asiondoke mkoani Geita bila kutatua mgogoro wa fidia kati ya wananchi na mgodi wa GGM pamoja na ule wa wachimbaji wadogo wa almasi wilayani Kishapu na mwekezaji (El Hillal Minerals Limited).
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG 
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Ardhi Mkoa Geita.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akikabidhi hati ya umiliki wa ardhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akikabidhi hati ya umiliki wa ardhi kwa mmoja wa wakazi wa Geita ambapo hati 168 zimekabidhiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Ardhi Mkoa Geita.
 Mmoja wa wakazi wa Mkoa Geita akipokea hati ya umiliki wa ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akikabidhi hati ya ardhi kwa mmoja wa wakazi wa Mkoa Geita.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto) akifuatilia hati mbalimbali za umiliki wa ardhi akiwa pamoja na Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) kwenye hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Ardhi Mkoa Geita.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Ardhi Mkoa Geita.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (wa watatu) akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili kulia) pamoja na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Geita (wa pili kushoto) kwenye uzinduzi wa Ofisi ya Ardhi Mkoa Geita.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.