LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHADEMA yajipanga kutetea majimbo yake "kuongeza mengine zaidi"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa Mara kimejipanga kikamilifu kuhakikisha kinatetea majimbo yake huku kikiongeza majimbo mengine mapya yaliyokuwa ngome ya vyama vingine ikiwemo CCM.

Katibu wa chama hicho Mkoa Mara, Mchele Kicheri (pichani juu) aliyasema hayo wakati akitangaza majina ya wagombea wa nafasi ya ubunge mkoani humo walioshinda kwenye kura za maoni na kuongeza kuwa wagombea wote wana ushawishi katika jamii na hivyo kuleta ushindaji mkali katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu 2020.
Na Asha Shaban, Mara
 Wajumbe wa mkutano wa kuwachagua wagombea Jimbo la Tarime Vijijini (Chadema) ambapo John Heche (kushoto) amepitishwa kutetea nafasi yake ya ubunge.
BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.