LIVE STREAM ADS

Header Ads

Katibu Mkuu ALAT apigwa butwaa utekelezaji wa miradi Buchosa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Elirehema Kaaya amepigwa butwaa kwa jinsi Watendaji katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema walivyomuelewa vyema Rais Dkt. John Magufuli na kutekeleza vyema miradi ya maendeleo.

Ni baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri hiyo ikiwemo ujenzi wa majengo 11 katika Hospitali mpya ya Wilaya, jengo la Ofisi za Halmashauri, vyumba vitatu vya madarasa pamoja na maktaba katika Shule ya Sekondari Nyehunge. 

Na George Binagi-GB Pazzo, BMGKatibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Elirehema Kaaya (kulia) akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Buchosa, Cyprian Luanda alipotembelea ujenzi wa jengo la Ofisi za Halmashauri hiyo.Jengo la maktaba katika Shule ya Sekondari Nyehunge lililojengwa kwa fedha za EP4R.Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Elirehema Kaaya akikagua maktaba katika Shule ya Sekondari Nyehunde.Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyehunge wakionyesha mbinu za ujifunzaji maabara.Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

SOMA>>> Ziara Katibu Mkuu ALAT Buchosa

No comments:

Powered by Blogger.