LIVE STREAM ADS

Header Ads

UVCCM tawi la CBE watangaza kumuunga mkono JPM

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) tawi la CBE Sokoine jijini Mwanza, imeazimia kumuunga mkono Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili ashinde kwa kishindo kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020.

Pamoja na kumuunga mkono Rais Magufuli, pia jumuiya hiyo imeazimia kutoa hamasa kwa ajili ya ushindi wa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge watakaopitishwa na vikao vya juu vya CCM. 

Maazimio hayo yalitolewa Jumapili Agosti 16, 2020 kwenye mkutano wa UVCCM tawi la CBE Sokoine ambapo mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa, Richard Kashilimu anayewakilisha Mkoa Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa, Richard Kashilimu alisema zawadi pekee kwa Rais Magufuli kutokana na utendaji kazi wake mzuri ni kumpigia kura ili ashinde kwa kishindo Uchaguzi Mkuu. Pia aliwataka vijana kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kumuombea kura pia mgombea urais Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi.
Katibu wa UVCCM tawi la CBE Sokoine alisema sababu za kumuunga mkono ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli, meli pamoja na umeme.
Viongozi wa UVCCM tawi la CBE Sokoine wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa, Richard Kashilimu (wa tatu kushoto).
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Viongozi na wanachama wa UVCCM tawi la CBE Sokoine wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa, Richard Kashilimu.
Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa, Richard Kashilimu pia alikabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya wa UVCCM tawi la CBE Sokoine.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.