LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkurugenzi UTPC "wananitungia uongo kunifukuza kazi"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan ameshangazwa na baadhi ya viongozi wa Klabu zinazounda muungano huo kumtungia mambo ya uongozi ili kumchafua na kumfukuzisha kazi.

Karsan ameyasema hayo Agosti 17, 2020 wakati akifungua mafunzo kwa wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) yanayolenga kuwajengea uwezo kuandika habari za magonjwa ya mlipuko ikiwemo Covid- 19 (Corona).

Akizungumza kwa masikitiko, Karsan alisema kuna baadhi ya viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari wasio waadilifu katika masuala mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za Klabu ambapo UTPC inapowahoji wanatafuta kila aina ya mbinu kumchafua wakidhani hiyo ndiyo njia rahisi ya kujitetea.

“Viongozi wengine ni wezi, wanachezea fedha, hawarejeshi ‘retirement’. Wananitungia kila aina ya uongo, wananipa maghorofa na majumba yote ya Mwanza bila kujua nina nyumba moja tu” alisema Karsan akisema yuko UTPC kwa ajili ya kuhakikisha jamii ya waandishi inanufaika.

Karsan pia alitoa wito kwa waandishi wa habari kuwachagua viongozi wenye heshima na wanaofuata taratibu za kiuongozi ili kusimamia vyema Klabu zao na si kuwachagua viongozi wataka vitu/ mali.

“Mwaka huu tuna uchaguzi wa viongozi wa bodi ya UTPC, ni matarajio yangu mtachagua viongozi wazuri ili waisimamie vyema UTPC” alisisitiza Karsan.

Kuhusu mafunzo hayo, Karsan alisema yamelenga kuwapa waandishi ujuzi na stadi za kazi wanapoandika habari za mlipuko ikiwemo Corona. “mbali na kwamba sisi ni waandishi lakini pia ni binadamu hivyo kuna suala la kuandika na kujikinga ili tusiambukizane miongoni mwetu ama katika familia zetu” alibainisha Karsan.

Aidha aliwakumbusha waandishi wa habari kuwa wamoja na kusaidiana kwenye shida na raha tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi wao hawashirikiani vyema. “Anzisheni utaratibu ikiwemo mabonanza ili muwe mnakutana mara kwa mara kwa ajili ya kuimarisha mahusiano yenu” Karsan alitoa rai kwa viongozi na wanachama wa MPC.

Pia Karsan aliwakumbusha waandishi wa habari hususani watangazaji kufanya kazi kwa weledi na kuacha mbwembwe zinazoharibu kazi yao “siku hizi watangazaji wanaimba, hawatangazi. Sasa kama wanaimba akina Diamond na Alikiba wafanye kazi gani? Watangazi wa Tanzania tusiimbe, bali tutangaze huku tukizingatia matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili”. 

Katika mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na UTPC, Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko aliwataka waandishi wa habari kuendelea kuandika habari za kuelimisha wananchi kuhusiana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Corona licha ya kwamba imepungua hapa nchini.Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs- UTPC), Abubakar Karsan akifungua mafunzo hayo katika ukumbi wa TRA Mkoa Mwanza.Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (Mwanza Press Cluc- MPC), Edwin Soko akitoa neno la utangulizi kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Edwin Soko wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan akifuatilia mafunzo hayo.Wanachama wa MPC wakifuatilia mafunzo hayo.Wanachama wa MPC wakiwa kwenye mafunzo hayo.Viongozi wa MPC wakifuatilia mafunzo hayo.Wanachama wa MPC wakiwa kwenye mafunzo hayo.

No comments:

Powered by Blogger.