LIVE STREAM ADS

Header Ads

NIPENI MITANO TENA MUONE NITAKACHOFANYA- DKT ANGELINE

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mgombea ubunge kupitia CCM katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Dkt. Angeline Mabula ametoa ahadi ya kumaliza kero zinazowakabili wananchi wa Kata ya Ilemela jimboni humo ikiwa watawachagua viongozi wanaotokana na chama hicho.

Dkt. Angeline aliyasema hayo wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu 2020 katika Kata ya Ilemela na kuongeza kuwa endapo CCM itapewa nafasi ya kuongoza kwa miaka mingine mitano, atajenga Zahanati pamoja na kuboresha Kituo cha Afya cha Lumala.

Aidha Dkt. Angeline alisema kama wananchi wa Kata ya Ilemela watachagua mafiga yote matatu kwa upande wa CCM (Rais, Mbunge na Diwani) atahakikisha ukarabati mkubwa unafanyika katika Shule ya Sekondari Lumala  na ile ya Msingi Mwambani.

Kwa upande wake mgombea udiwani wa Kata hiyo ya Ilemela, Wilbard Kilenzi alisema katika miaka mitano wameshughulikia kero za ardhi ambapo wananchi wengi wamepimiwa viwanja vyao na waliokuwa wakidai fidia wengi wamelipwa.

Kilenzi alitolea mfano mgogoro wa ardhi katika eneo la Nyakuguru ambapo Serikali kupitia Dkt. Angeline walimaliza mgogoro huo na hivyo kuomba wananchi wamchague tena kuwa mbunge wao.

Kwa upande wake Meneja kampeni wa Dkt. Angeline, Kazungu Safari aliwataka wananchi wa Kata ya Ilemela wasije wakarudia kosa la kumrudisha diwani wa upinzani kwa sababu Kilenzi bado anatosha.
Imeandaliwa na Tonny Alphonce, Ilemela

No comments:

Powered by Blogger.