LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAJALIWA awakumbuka waliofariki MV. NYERERE

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa Septemba 23, 2020 amefika kutoa heshima katika makaburi ya pamoja ya baadhi ya abiria waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kilichozama Septemba 20, 2018 katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa akiweka mashada kwenye makaburi hayo.
Viongozi wa dini wakiongoza dua.
Mnara wa makaburi ya pamoja ya baadhi ya abiria waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kilichozama katika Kisiwa cha Ukara kikitokea Kisiwa cha Bugolora wilayani Ukerewe ambapo abiria 227 walifariki.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa pia alitembela Kituo cha Afya Bwisya kilichoboreshwa na Serikali na kufikia hadhi ya Hospitali ya Wilaya. Katika Mkutano wake wa hadhara Majaliwa alitangaza kusudio la Rais Dkt. John Magufuli kukipandisha hadhi Kituo cha Afya Bwisya kuwa na hadhi ya Hospitali ya Wilaya na Hospitali ya Wilaya Ukerewe Nansio kuwa na hadhi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Akiwa katika Kisiwa cha Ukara, Majaliwa alifanya Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu na kuwaombea kura wagombea wa CCM kuanzia udiwani, ubunge na urais.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.