LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAGUFULI AWAVURUGA WAPINZANI MWANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi baada ya kuwasili Magu mkoani Mwanza akitokea mkoani Mara, Septemba 06, 2020. 
Dkt. Magufuli ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuwachagua viongozi wa CCM ili wakakamilishe utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo walioianza katika awamu ya kwanza ya uongozi wake.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mwanza, Antony Diallo akisalimia wananchi.
Mgombea ubunge jimbo la Nyamagana (CCM), Stanslaus Mabula akisalimia wananchi na kuomba kura.
Wagombea ubunge kupitia CCM katika majimbo mbalimbali mkoani Mwanza wajitambulisha kwa wananchi.
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mwanza, Antony Diallo (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) ni miongoni mwa waliojitokeza kumpokea mgombea urais CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akitokea mkoani Mara. Dkt. Magufuli anatarajiwa kuwa na Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu katika uwanja wa CCM Kirumba Jumatatu Septemba 07, 2020.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Umati wa wananchi wamejitokeza kwa wingi kumpokea mgombea urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli kuanzia Magu mjini, Kisesa, Nyanguge, Nyakato, Buzuruga pamoja na Mabatini.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.