LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHY TOWN VIP WATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO BUHANGIJA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wanachama wa Makundi ya Whatsapp Mjini Shinyanga likiwemo Group maarufu kwa la ‘SHY TOWN VIP’ linaloundwa na wadau wa maendeleo wametembelea Kituo cha Kulelea Watoto wenye ulemavu cha Buhangija na kutoa zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, taulo za kike ‘pedi’,sabuni,juisi,soda,toilet papers,pipi,chumvi,keki kisha kucheza nao muziki. 

Ziara hiyo ya Wanachama wa Makundi ya Mtandao wa Whatsapp 'Members wa Whatsapp Groups' takribani 8 yaliyodumu kwa muda wa miaka mitatu sasa iliyofanyika Jumamosi Oktoba 3,2020 ikiwa ni sehemu ya sherehe ya Wanachama wa Magroup ya Whatsapp Mjini Shinyanga ambapo pia leo jioni watakutana kwa ajili ya kula chakula cha pamoja na burudani mbalimbali. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lulekia Co. Ltd, Ansila Benedict amesema wameamua kutembelea kituo cha Buhangija ili kuonesha upendo kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo wakiwemo watoto wenye ualbino,wasiosikia ‘viziwi’ na wasioona. 

“Leo tuna sherehe ya wanachama wa Makundi ya Whatsapp ‘SHY TOWN VIP’, baadhi yetu tumefika hapa ili kukabidhi zawadi kwa watoto na baadaye tutaendelea na sherehe pale La Prince Pub. Tumekuja na pia na keki ikiwa ni ishara ya upendo kwa watoto wetu”,amesema Ansila. 

Kwa upande wake Vivian Zabron kutoka Dawati la Jinsia na watoto Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga ambaye ni miongoni mwa wanachama wa Group la SHY TOWN VIP amesema kila mmoja katika jamii ana wajibu wa kulinda watoto,kuwajali na kuwapatia haki wanazostahili na pindi haki za watoto zinapokiukwa ni vyema wananchi wakatoa taarifa kwenye vyombo vya dola. 

Nayo Kampuni ya Vinywaji TBL, kupitia kwa mwakilishi wao TofeeUptown imenunua umeme wa shilingi 50,000/= kwa ajili ya kituo cha kulelea watoto cha Buhangija. 

Mwalimu Mlezi katika kituo cha kulelea watoto Buhangija , Anna Onesmo amewashukuru watumiaji hao wa mitandao ya kijamii kufika katika kituo hicho akisema wameonesha upendo wa hali juu kufariji watoto na kuomba wadau wengine kuendelea kutembelea watoto hao. 
Kiongozi wa Msafara wa Wanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga ' Shy Town VIP' waliotembelea kituo cha kulelea watoto cha Buhangija Mjini Shinyanga, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lulekia Co. Ltd, Ansila Benedict akizungumza wakati wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga wakikabidhi zawadi kwa watoto hao Jumamosi Oktoba 3,2020.
Mwalimu Mlezi katika kituo cha kulelea watoto Buhangija , Anna Onesmo akizungumza wakati wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga 'Shy Town VIP' wakikabidhi zawadi kwa watoto hao. 
Vivian Zabron kutoka Dawati la Jinsia na watoto Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga ambaye ni miongoni mwa wanachama wa Group la SHY TOWN VIP akizungumza wakati wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga 'Shy Town VIP' wakikabidhi zawadi kwa watoto hao. 
Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lulekia Co. Ltd, Ansila Benedict akikabidhi zawati ya juisi zilizotolewa na wanachama wa Makundi ya Whatsapp Shinyanga 'Shy Town Vip' kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga Jumamosi Oktoba 3,2020. 
Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lulekia Co. Ltd, Ansila Benedict akikabidhi zawati ya juisi zilizotolewa na wanachama wa Makundi ya Whatsapp Shinyanga 'Shy Town Vip' kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lulekia Co. Ltd, Ansila Benedict akikabidhi zawati ya toilet papers zilizotolewa na wanachama wa Makundi ya Whatsapp Shinyanga 'Shy Town Vip' kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga. 
Mc Zeze ' Mwalimu Zezema Shilungushela' ambaye ni miongoni mwa wanachama wa Magroup ya Whatsapp 'Shy Town VIP' akizungumza katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija Mjini Shinyanga. 
Mc Ice ' Sauti ya Simba' ambaye ni miongoni mwa wanachama wa Magroup ya Whatsapp 'Shy Town VIP' akifurahia na watoto. 
Wanachama wa Magroup ya Whatsapp 'Shy Town VIP' wakifurahia na watoto kwa kucheza muziki. 
Wanachama wa Magroup ya Whatsapp 'Shy Town VIP' wakifurahia na watoto kwa kucheza muziki. 
Wanachama wa Magroup ya Whatsapp 'Shy Town VIP' wakifurahia na watoto kwa kucheza muziki. 
Wa tatu kulia ni Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp 'Shy Town VIP', TofeeUptown akikata keki na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija iliyoandaliwa na Wanachama wa Makundi ya Whatsapp Shinyanga kama ishara ya upendo kwa watoto hao. 
Wa tatu kulia ni Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp 'Shy Town VIP', TofeeUptown akikata keki na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija iliyoandaliwa na Wanachama wa Makundi ya Whatsapp Shinyanga kama ishara ya upendo kwa watoto hao. 
Wa tatu kulia ni Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp 'Shy Town VIP', TofeeUptown akimlisha keki mtoto katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija. 
MC ICE ambaye ni Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp 'Shy Town VIP', akimlisha keki mtoto katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija. 
Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga 'Shy Town VIP', Grace Mng'ong'o ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear akimlisha keki mtoto katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija. 
Eva Chaulema kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Shinyanga ambaye ni Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp 'Shy Town VIP', akimlisha keki mtoto katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija. 
Mkurugenzi wa Malunde 1 Blog, Kadama Malunde ambaye ni Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp 'Shy Town VIP', akimlisha keki mtoto katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija. 
Msanii Patrick akitoa burudani katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija. 
Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga 'Shy Town VIP', Zezema Shilungushela akikabidhi taulo laini kwa mtoto katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija. 
Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga 'Shy Town VIP', Hanifa akigawa pipi kwa watoto katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija. 
Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga 'Shy Town VIP', Leila akigawa pipi kwa watoto katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija.


Wanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga 'Shy Town VIP' wakipiga picha ya pamoja na watoto katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija. 
Wanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga 'Shy Town VIP' wakipiga picha ya pamoja na watoto katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija. 
Na Kadama Malunde - Malunde 1 Blog

No comments:

Powered by Blogger.