LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jumuiya ya Maridhiano yawatahadharisha wanasiasa “Tume ya Uchaguzi”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Jumuiya ya Maridhiano Tanzania imewahimiza wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020 kuhakikisha wanajiepusha na viashiria vya uvunjifu wa amani ikiwemo kukubali matokeo baada ya Uchaguzi. 

Viongozi wa jumuiya hiyo ngazi ya Mkoa Mwanza wametoa kauli hiyo Oktoba 20, 2020 wakati wakizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa watanzania wote wanapaswa kulinda amani kwa kusimamia misingi ya haki, utu na upendo. 

Itakumbukwa kuwa majukumu makubwa ya Jumuiya ya Maridhiano Tanzania ni pamoja na usuluhishi wa migogoro na changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri suala la amani nchini.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.