MPC yazindua rasmi akaunti ya Mfuko wa Kusaidiana "MPC Solidarity Fund"
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (Mwanza Press Club- MPC) kimezindua rasmi akaunti ya benki ya Mfuko wa Kusaidiana katika Maafa na Starehe (MPC Solidarity Fund) hatua itakayowasaidia wanachama wake kupata msaada wa haraka wanapokuwa na uhitaji.
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko amesema huo ni mfumo rasmi ambao utaiondoa klabu kwenye utaratibu wa kizamani wa kutegemea michango pindi mwanachama anapopata tatizo huku akitoa rai kwa waandishi wa habari kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba kwa ajili ya utatuzi wa changamoto mbalimbali zinapojitokeza.
Naye mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi huo ambaye ni Mwenyekiti Mstaafu wa MPC, Deus Bugaywa amepongeza hatua iliyofikiwa na kuwahimiza wananchama wa MPC kutoa michango yao kwa wakati ili kuimarisha mfuko huo huku akitoa rai kwa waandishi wengine nchini kupitia klabu zao kuiga utaratibu mzuri huku.
Aidha amewapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kutunisha mfuko huo ikiwemo taasisi ya The Desk & Chair Foundation na Hospitali ya Uhuru na kutoa rai kwa wadau wengine kujitokeza kuunga kuunga mkono jitihada hizo.
Tazama matukio mbalimbali katika picha kwenye Uzinduzi Rasmi wa akaunti ya Mfuko wa Kusaidiana wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza iliyofanyika Jumanne Oktoba 2020 katika Ofisi ya Benki ya NBC tawi la Nyanza jijini Mwanza.
#BMGHabari
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mstaafu wa MPC, Deus Bugaywa (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa akaunti ya mfuko wa kusaidia wa klabu hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko na kushoto ni Meneja wa benki ya NBC, William Mazungu.
SOMA>>> Matukio mbalimbali kuhusu MPC
No comments: