LIVE STREAM ADS

Header Ads

Baada ya wanafunzi kulalamikia unyanyasi wa kingono, DC aagiza Chuo kifungwe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Baada ya wanafunzi wa kike katika chuo cha St. Christina kilichopo Wilaya Bunda mkoani Mara kulalamikia vitendo vya udhalilishaji wa kingono kutoka kwa mmiliki wa chuo hicho, Mkuu wa Wilaya hiyo Mwl. Lydia Bupilipili ameagiza kifungwe.

Bupilipili ametoa maamuzi hayo Oktoba 2020 akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi wilayani Bunda kufuatia uchunguzi uliofanywa chuoni hapo kubaini mapungufu kadhaa ikiwemo chuo kuwa na mazingira mabovu ya kufundishia na ufundishaji na kuagiza mkurugenzi huyo akamatwe kwa ajili ya hatua za kisheria.

Wanafunzi wa kike walivunja ukimia na kulalamikia unyanyasaji wa kingono chuoni hapo Oktoba 15, 2020 kupitia vyombo vya habari.
#BMGHabari
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.