LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanafunzi Bunda wamtuhumu Mmiliki wa Chuo kuwanyanyasa kingono

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wanafunzi wa Chuo cha St. Christina kilichopo Kata ya Kunzugu wilayani Bunda mkoani Mara wamevunja ukimya na kulalamikia vitendo vya ukatili wa kingono wanavyofanyiwa na mmiliki wa chuo hicho.

Baadhi ya wanafunzi wa kike chuoni hapo wanasema mmiliki huyo amekuwa akiwataka kimapenzi na wanapogoma huwatishia kuwa atawaharibia vyeti baada ya kuhitimu masomo.
#BMGHabari
Mkuu wa Wilaya Bunda, Mwl. Lydia Bupilipili amefika chuoni hapo na kusikiliza malalamiko ya wanafunzi hao na kuahidi uchunguzi wa haraka kufanyika ili hatua stahiki zichukuliwe.
Wanafunzi wa chuo hicho walitoa malalamiko ya kunyanyaswa kingono wakisisitiza hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa mmiliki huyo wa chuo.
Wanafunzi wa chuo hicho wakiwasilisha kero zao kwa Mkuu wa Wilaya Bunda, Mwl. Lydia Bupilipi alifefika chuoni hapo Oktoba 16, 2020.
Mkuu wa Chuo cha St. Christina, Mwl. Msiro Mshandete (kushoto) akitoa maelezo ya awali kwa Mkuu wa Wilaya Bunda, Mwl. Lydia Bupilipi (kulia) kuhusiana na malalamiko ya wanafunzi kunyanyaswa kingono na mmiliki (Mkurugenzi) wa chuo hicho.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wakiwa nje ya bweni.
Mwonekano wa ndani wa bweni la wavulana chuoni hapo.
Sehemu ya mwonekano wa ndani wa bweni la wasichana.
Wanafunzi wa chuo hicho wanasema shimo hili la maji taka linapojaa hupewa adhabu ya kuyaondoa humu.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.