LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakazi wa Ukerewe waipokea kwa shangwe MV Ukara II “Hapa Kazi Tu”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amezindua rasmi safari za kivuko kipya cha MV. Ukara II “Hapa Kazi Tu” ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 4.2. 

Kivuko hicho ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kivuko cha MV. Nyerere kuzama Septemba 20, 2018 katika kisiwa cha Ukara kikitokea kisiwa cha Bugorola wilayani Ukerewe. Uzinduzi huo ulifanyika Oktoba 19, 2020 katika kisiwa cha Ukara. 

Baadhi ya wakazi wa Ukerewe wamepokea kwa furaha kivuko hicho wakisema kitaondoa adha ya usafiri na kuimarisha shughuli za kiuchumi baina ya visiwa vya Ukara na Bugorola.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Viongozi wa dini wakifanya maombi katika kivuko cha MV. Ukara II "Hapa Kazi Tu". Wengine ni viongozi wa Serikali na vyama vya siasa.
Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto) akimpongeza Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro Marine (kulia) kwa kutengeneza kivuko hicho kwa viwango vya kimataifa.
Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kivuko cha MV. Ukara II.
Wakazi wa Ukara walijitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa kivuko hicho.
Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elius Mwakalinga.
Mtendaji Mkuu TEMESA, Japhet Masele.
Wakazi wa Ukara wakiwa kwenye hafla fupi ya mapokezi ya kivuko cha MV. Ukara II.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Viongozi mbalimbali.
Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati), Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) na Mkuu wa Mkoa Mara, Adam Malima Ukushoto) wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wakazi wa Ukara wakifurahia ujio wa Kivuko cha MV. Ukara II.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.