LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAOJIHUSISHA NA UKATILI WA KIJINSIA WASIONEWE HURUMA- RC MONGELLA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Johm Mongella ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia wale wote wanaobainika kutenda vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto. 

Mongella alitoa kauli hiyo Novemba 25, 2020 kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupiga ukatili wa kijinsia uliofanyika kwa Mkoa Mwanza katika uwanja wa Furahisha Manispaa ya Ilemela. 

Alisema wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia lazima washughulikiwe bila huruma ili iwe fundisho kwa wengine na kwamba hatua hiyo itasaidia kutokomeza tabia hiyo ovu kwani haiwezekani waharibu maisha ya wanajamii. 

Kufuatia maagizo hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza Muliro Jumanne alionya kuwa jeshi hilo litaelekeza nguvu iliyotumika kupambana na ujambazi katika kupambana na watu wanaojihusisha na ukatili wa kijinsia. 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema shirika hilo limewajengea uwezo wanaharakati zaidi ya elfu mbili ili kutoa elimu na msaada wa kisheria bure katika ngazi ya jamii na hivyo kusaidia mapambano dhidi ya ukatili wakijinsia.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Wanahabari wakinasa matukio kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Muliro Jumanne.
Wanaharakati wa shirika la KIVULINI wakitoa uafafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akuhusiana na shughuli zinazofanywa na shirika hilo katika kupambana na ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Mkoa Mwanza (katikati) akiwa katika banda la shirika la KIVULINI kuona shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na shirika hilo katika kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akitembelea mabanda mbalimbali katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.