LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YATAMBUA MCHANGO WA WATAALAMU WA JIOLOJIA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wataalamu wa Jiolojia na kutoa wamepongezwa kutokana na mchango wao katika kuchangia ongezeko la fedha za kigeni pamoja na pato la Taifa kupitia shughuli mbalimbali katika sekta ya madini. 

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ametoa pongezi hizo wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wajiolojia Tanzania (TGS), unaofanyika jijini Mwanza kwa siku tano kuanzia Novemba 26, 2020. 

Amesema mchango wa wataalamu hao umesaidia sekta ya madini kuliingizia Taifa fedha za kigeni kiasi cha shilingi bilioni 2.7 huku makusanyo yakiongezeka kutoka shilingi bilioni 168 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 527 mwaka 2019/2020. 

Mongella pia amepongeza mchango wa wataalamu hao wa jiolojia kwa namna wanavyochochea maendeleo ya sekta ya madini hususani kwa wachimbaji wazawa hatua iliyosaidia kuibua mabilionea nchini akiwemo bilionea Saniniu Kuryan Laizer. 

Naye Rais wa TGS, Profesa Abdulkarim Mruma amesema juhudi malimbali zinazofanywa katika sekta ya madini zinaweza kusaidia mchango wa sekta hiyo katika pato la Taifa kuongezeka hadi kufikia asilimia 10 kabla ya mwaka 2025 kutoka asilimia 5.2 ya sasa. 

Katika mkutano huo TGS imetoa tuzo mbili za heshima, moja ikienda kwa Mjiolojia Faustus Rutahindurwa aliyesaidia tafiti mbalimbali katika mgodi wa mchimbaji madini Saniniu Kuryan Laizer ambaye hivi karibuni alitangazwa bilionea baada ya kuuza kiasi kikubwa cha madini ya Tanzanite na nyingine kwa mchimbaji huyo (Saniniu Kuryan Laizer) ikiwa ni sehemu ya kuthamini mchango wao katika sekta ya madini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Rais wa Chama cha Wajiolojia Tanzania (TGS), Profesa Abdulkarim Mruma.
Katibu Mtendaji chama cha wajiolojia Tanzania (TGS), Dkt. Elisante Mshiu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akikabidhi tuzo kwa Mjiolojia Faustus Rutahindurwa (kushoto) iliyotolewa na TGS ili kutambua mchango wake katika sekta ya madini.
Mwakilishi wa kampuni ya Global Fortune (wa pili kulia) akimkabidhi Mjiolojia Faustus Rutahindurwa (wa pili kushoto) nyaraka za kiwanja kilichopi jijini Mwanza ikiwa ni zawadi ya kutambua mchango wake.
Wajiolojia mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio (kulia) akimweleza Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo ikiwemo mpango wake wa kusambaza gesi katika mikoa mbalimbali nchini.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) pia alitembelea banda la TANESCO kuonesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za shirika hilo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.