LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHEIKH WA MWANZA AONYA KUHUSU MAANDAMANO

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa Mwanza limewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwemo kushiriki maandamano baada ya Uchaguzi Mkuu kwani kufanya hivyo kunaweza kuhatarisha maisha yao.

Sheikh wa Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke ametoa rai hiyo Oktoba 31, 2020 wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Maulidi (mazazi ya Mtume) akiunga mkono tamko la Mufti wa Tanzania la kupinga maandamano yaliyotangazwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani.

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alizipongeza taasisi za dini kwa namna zilivyoshiriki kuliombea Taifa ili kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unafanyika kwa amani na utulivu.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waamini mbalimbali wa dini ya kiislamu wakiwa kwenye maadhimisho ya Maulidi mkoani Mwanza.
Sheikh Mkuu wa Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto).
Mkuu wa Mkoa Mwanza akitoa salamu zake kwenye maadhimisho ya Maulidi 2020 jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza (kulia) akiwasili kwenye maadhimisho hayo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.