MKUU WA WILAYA MISUNGWI AZINDUA MSIMU MPYA WA PAMBA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Sweda akiwa ameambatana na viongozi na watendaji mbalimbali wilayani Misungwi, alizundua msimu huo Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Maganzo Kata ya Mondo na kusisitiza kwamba wananchi wote wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo.
Alisema kila mwenye shamba lazima akalime kwani ni aibu kukuta vijana wanacheza bao, karata ama kunywa pombe muda wa shamba huku wengine hususana akina mama wakiwa mashambani.
“Wakamatwe wapelekwe wakalime, ikifanyika hivyo kila mtu atafanya kazi kwa bidii kwa sababu hakuna wa kuja kukusaidia” alisisitiza Sweda.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akipanda pamba akiwa na watendaji pamoja na wakulima katika Kata ya Mondo kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa zao la pamba ulioanza Novemba 15 hadi Disemba 15, 2020.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akilima kwa jembe la kukokotwa na ng'ombe ikiwa ni maandalizi ya kupamba pamba.
Katibu Tawala Wilaya Misungwi, Petro Sabatto ni miongoni mwa viongozi walioshiriki kuhamasisha msimu wa ulimaji pamba 2020/21.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
SOMA>>> DC MISUNGWI AKUTWA SHAMBANI
No comments: