LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko aushukia jumla jumla mgodi wa North Mara, Nyamongo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameunya uongozi wa mgodi wa North Mara uliopo Nyamongo Wilaya ya Tarime mkoani Mara, baada ya kujenga mtambo wa kusafisha maji yanayotoka kwenye bwawa la tope sumu (TSF) bila kufuata utaratibu. 

Waziri Biteko amesema mgodi huo ambao unaendeshwa kwa ubia baina ya Serikali na kampuni ya Barrick kupitia kampuni tanzu ya Twiga umekiuka sheria ya madini kwa kuleta kampuni kutoka nje ya nchi ili kujenga mtambo huo licha ya kunyimwa kibali kutoka Tume ya Madini. 

“Tunataka hizi kazi zifanywe na watanzania ili manufaa ya madini yaweze kufungamanishwa na uchumi mwingine, sasa kampuni hii ilitangaza tenda nje ya nchi bila kufuata utaratibu na hata waliponyimwa kibali bado waliendelea na mchakato wao” ameeleza Biteko na kuongeza kuwa kwa kosa hilo mgodi unaweza kupigwa faini kuanzia dola milioni tano na kuendelea.

Aidha Biteko ameutaka mgodi huo kuanza kutoa fedha za huduma za jamii (CSR) kwani kwa takribani miaka miwili iliyopita haujatoa fedha hizo ambapo amemwelekeza Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima kuitisha kikao cha maridhiano baina ya Halmashauri na mgodi huo ili fedha hizo zianze kulipwa. 

Katika hatua nyingine Waziri Biteko amesema wale wote wanaostahili kulipwa fidia ili kupisha maeneo yao kwa ajili ya shughuli za mgodi watalipwa na madai yao yanafanyiwa kazi huku akirejea msimamo wa Serikali kwamba waliotegesha hawatalwipa fidia.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na viongozi mbalimbali mkoani Mara kabla ya kutembelea mgodi wa North Mara Nyamongo.
Viongozi mbalimbali mkoani Mara pamoja na Wizara ya Mdini wakimsikiliza Waziri wa Madini, Doto Biteko.
Viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mara, Adam Malima wakati akitoa taarifa fupi ya hali ya uchimbaji madini mkoani humo.
Viongozi mbalimbali.
Bwawa la tope sumu (TSF) katika mgodi wa North Mara.
Mwakilishi wa mgodi wa North Mara (kulia) akieleza jitihada zinazofanywa na mgodi huo kudhibiti maji kutoka kwenye bwawa la tope sumu.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali kukagua eneo ulipojengwa mtambo wa kusafisha maji kutoka kwenye bwawa la tope sumu (TSF).
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.