LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yawashukia mafundi simu “wakasome”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Serikali imewataka mafundi simu nchini kujiendeleza kielimu ili kupasa sifa stahiki za kupata cheti cha kitaaluma pamoja na leseni ya biashara kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo. 

Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainabu Chaula ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao na mafunzi simu Kanda ya Ziwa kilichofanyika Disemba 17, 2020 jijini Mwanza. 

Dkt. Chaula alisema tayari Serikali imeandaa mtaala kwa ajili ya mafunzo kwa ajili ya mafundi simu na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo kwa kujisomesha wenywe badala ya kutegemea kusomeshwa na Serikali.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainabu Chaula (katikati) akizungumza kwenye kikao na mafundi simu Kanda ya Ziwa. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Jonas na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu TCRA Mhandisi James Kilaba.
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainabu Chaula aliipongeza TCRA kwa kutoa mafunzo na kuwasajili mafundi simu zaidi ya 200 Kanda ya Ziwa na kutoa rai kwa mafundi hao kutumia umoja huo kwa shughuli za kimaendeleo ikiwemo kuanzisha 'sakosi'.
Mafundi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainabu Chaula.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Jonas aliwahimiza mafundi simu kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kujiepusha na  vitendo vya uhalifu akisema mafundi simu wana mchango mkubwa kwenye ulinzi wa taifa.
    Tayari takribani mafundi simu 500 wamesajiliwa kote nchini lengo likiwa ni kuwatambua na kuwawezesha kunufaika na fursa mbalimbali.
Baada ya Serikali kurasimisha sekta ya mafundi simu, msisitizo umetolewa wakajiendeleze kielimu ili kupata vyeti vya kitaaluma pamoja na leseni za kufanya biashara hiyo kihalali.
Mkurugenzi Mkuu TCRA, Mhandisi James Kilaba alisema awali mafundi simu walikuwa wanafanya kazi kiholela huku wengine wakivunja sheria ambapo mamlaka hiyo iliona badala ya kuwakamata ni vyema kuwaelimisha na kuwasajili hatua ambao imewasaidia kujitambua na kufanya kazi kihalali kwa kuzingatia sheria.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo alisema mamlaka hiyo inawajengea uwezo mafundi simu ili kufanya kazi kwa weledi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Simu Kanda ya Ziwa, Maguwa Manyanda aliomba Serikali kuwasaidia ili taasisi za kibeki zitambue sekta ya mafundi simu na kupata sifa ya kukopesheka ili kukuza mitaji na kuendeleza zaidi shughuli zao.
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainabu Chaula.
Mafundi simu Kanda ya Ziwa.
Mafundi simu kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Simu Kanda ya Ziwa, Maguwa Manyanda (kulia) akimweleza Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainabu Chaula shughuli zinafanywa na umoja huo.
Picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.