LIVE STREAM ADS

Header Ads

Usicheze na Majaliwa, Mkurugenzi aliyembishia aumbuka

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametoa muda wa siku saba kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Jiji la Mwanza, Chato, Msalala na Kahama kujieleza ni kwa nini wamenunua magari ya kifahari kinyume na itifaki zao. 

Majaliwa ametoa agizo hilo Disemba 17, 2020 wakati akizungumza kwenye kikao kazi na viongozi mbalimbali mkoani Mwanza wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wabunge, madiwani pamoja na wakuu wa idara. 

Aidha Majaliwa ameonesha kukerwa na hatua ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kutoa tenda ya ujenzi wa stendi ya mabasi na maegesho ya malori Nyamhongolo kwa mkandarasi aliyedai gharama za juu kiasi cha shilingi bilioni 28 badala ya aliyedai shilingi bilioni 22. 

Katika hatua nyingine Majaliwa amewataka wataalamu na viongozi mbalimbali wa halmashauri wakiwemo madiwani kuhakikisha wanasimamia vyema matumizi ya fedha za Serikali kwa kutoruhusu matumizi makubwa yasiyoendana na uhalisia.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.