LIVE STREAM ADS

Header Ads

Viongozi wa mikoa watakiwa kusimamia zoezi la kuwatambua wenye ulemavu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wametakiwa kuhakikisha wanasimamia vyema zoezi la kuwatambua watoto wenye mahitaji maalumu linalotarajiwa kuanza Januari 9-21, 2021. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo alitoa agizo hilo jijini Mwanza Januari 04, 2021 wakati akifungua mafunzo elekezi kwa maafisa maendeleo, ustawi wa jamii, elimu maalumu pamoja na wauguzi watakaoshiriki kwenye utekelezaji wa zoezi hilo. 

Naye Mkurugenzi wa Elimu OR-TAMISEMI, Mwl. Julius Nestory alibainisha kuwa zoezi hilo linalenga kuwabaini watoto wenye umri kati ya miaka minne hadi sita ambao wana ulemavu, aina na kiasi cha ulemavu wao ili waandikishwe shule kulingana na mahitaji yao kielimu huku pia likiondoa dhana ya muda mrefu ya baadhi ya walemavu kufichwa majumbani na kukosa huduma na mahitaji wanayostahili.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo.
Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza kwenye mafunzo hayo ambapo pia aliwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuwabaini watoto wote wenye ulemavu Tanzania Bara ambao wana umri kati ya miaka minne hadi sita kwa ajili ya kuandikishwa shule kulingana na mahitaji yao.
Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka Halmashauri zote Tanzania Bara.
Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo akipokea ufafanuzi wa vifaa vitakavyotumika kwenye zoezi la kuwatambua watoto wenye mahitaji maalumu/ wenye ulemavu.
Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo (wa pili kulia) akipokea ufafanuzi wa vifaa vitakavyotumika kwenye zoezi la kuwatambua watoto wenye mahitaji maalumu/ wenye ulemavu. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.