LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tarime walia na uhaba wa mbegu bora

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Helena Magabe, Simiyu
AFISA Kilimo Halmashauri ya Wlaya ya Tarime mkoani Mara, Silvanus Gwiboha amesema kuna uhaba wa mbegu bora wilayani humo hali inayowapelekea wakulima kuingia gharama kubwa ya kununua mbegu kutoka nchi jirani ya Kenya.

Akizungumza katika siku ya mkulima iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti na kilimo (TARI) yaliyofanyika viwanja vya Nanenane mkoani Simiyu, Gwiboha alisema upatikanaji wa mbegu bora umekuwa mgumu zaidi kufuatia ugonjwa janga la corona kwani bado mipaka haijafunguliwa.

Aidha aliiomba Wizara ya Kilimo kuanzisha maduka rasmi ya kilimo ambayo yatakuwa na mbegu za uhakika.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Benson Kilangi ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Simiyu, huo Anthony Mtaka alisema uchaguaji wa mbegu bora ni suala la msingi.

Aliwaomba wakulima kuwa macho na mabadiliko ya keknolojia kwa kuhakikisha wanachagua mbegu bora na sio bora mbegu.

Alisema zipo mbegu za kila aina na bei tofauti tofauti zenye mvuto na urembo pamoja na 'package' za kuvutia lakini hazina ubora.

Kwa upande wao wakulima walishukuru TARI kwa kuwawezesha kujifunza kwa vitendo kutumia mbegu bora pamoja na kutembelea shamba darasa lenye mazao mbalimbali.

Ismail Mohamed Mariba alisema amefurahishwa kuona ulezi lishe mweupe na anaomba mbugu hiyo isambazwe kwa wakulima wengi ambapo pia amejifunza kutumia mbolea na mbegu bora.

Aidha alishukuru TARI kwa kuuza mbegu kwa gharama nafuu kwani alinunua mbegu za mahindi Tarime kwa bei ya shilingi 12,000 lakini kwa TARI alinunua kwa shilingi 8,000.

TARI ni taasisi ya utafiti wa kilimo iliyojikita kuandaa mbegu bora kwa jili ya kufundisha wakulima kwa vitendo katika shamba darasa katika eneo la Nyakabindi mkoani Simiyu lenye mazao kama vile viazi lishe, mtana mweupe, ulezi mweupe na mazao mengine mengi.

Mafunzo hayo ya siku moja yaliyoandaliwa ikiwa ni siku ya maadhimisho ya mkulima yalihusisha wakulima kutoka Mara, Simuyu pamoja na Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Benson Kilangi akizungumza kwenye hafla hiyo.
Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya Tarime, Silvanus Gwiboha akikabua mbegu.

No comments:

Powered by Blogger.