LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kikosi kazi Mwanza kuanza ukusanyaji kodi ya majengo, ardhi na machinga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Zoezi la ukusanyaji kodi ya majengo, ardhi na vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo linatarajiwa kuanza kwa ukaguzi maalum jumatatu Februari 15, 2021 katika Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kabla ya kuendelea katika Halmashauri zingine.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella wakati akizungumza na wanahabari na kubainisha kwamba zoezi hilo litasimamiwa na kikosi kazi (task force) na hivyo kuwataka wananchi na watendaji mbalimbali kutoa ushirikiano ili kutekeleza vyema zoezi hilo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akitoa taarifa kwa umma kuhusiana na zoezi la ukusanyaji kodi ya majengo, ardhi na vitambulisho vya machinga katika Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela. 
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.