LIVE STREAM ADS

Header Ads

Loh! Wanafamilia wamshushia kipigo kaka yao, ulitusaliti

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Muda mchache baada ya Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella kukabidhi hati ya nyumba kwa mjane Prucheria Balilemwa (79) mkazi wa Kilimahewa wilayani Ilemela ambaye nyumba yake iliuzwa kiutata, wanafamilia wamemshushia kipigo kaka yao kwa madai kwamba alishiriki njama za nyumba hiyo kuuzwa.

Kabla ya mkasa huo, Mongella amemkabidhi hati mjane huyo ambaye kwa sasa anasumbuliwa na maradhi ya kupooza baada ya nyumba aliyoachiwa na marehemu mmewe kuuzwa katika mazingira ya kutatanisha.

Kwa muda mrefu mjane huyo amekuwa akihangaika kupata haki hiyo na malalamiko yalipomfikia Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella kuyashughulikia.

Jumapili Februari 14, 2021 Mongella alifika nyumbani kwa mjane huyo Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Ilemela na kutoa siku tatu kwa Kaimu Kamishna wa Ardhi Mkoa Mwanza kuhakikisha hati hiyo inarejeshwa ili amkabidhi ambapo agizo hilo limefanyiwa kazi na Jumatato Februari 17, 2021 bibi huyo amepata haki yake.

Mwaka 1995 mme wa bibi huyo aitwaye Poncian Balilemwa alifariki dunia ambapo miaka mitatu baadae yaliibuka madai ya uwepo wa deni alilokopa benki mwaka 1984 yaliyosababisha mwaka 2003 nyumba aliyoiacha kuuzwa kwa njia ya mnada ambao ulilalamikiwa kugubikwa na utata.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.