LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella arejesha hati ya nyumba ya mjane iliyouzwa kiutata

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) amemkabidhi hati ya nyumba mjane Prucheria Balilemwa (aliyekaa) baada ya nyumba aliyokuwa ameachiwa na marehemu mmewe kuuzwa katika mazingira ya kutatanisha.

Kwa muda mrefu bibi huyo mwenye miaka 79 amekuwa akihangaika kupata haki hiyo na malalamiko yalipomfikia Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella kuyashughulikia.

Jumapili Februari 14, 2021 Mongella alifika nyumbani kwa mjane huyo Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Ilemela na kutoa siku tatu kwa Kaimu Kamishna wa Ardhi Mkoa Mwanza kuhakikisha hati hiyo inarejeshwa ili amkabidhi ambapo agizo hilo limefanyiwa kazi na Jumatato Februari 17, 2021 bibi huyo amepata haki yake.

Mwaka 1995 mme wa bibi huyo aitwaye Poncian Balilemwa alifariki dunia ambapo miaka mitatu baadae yaliibuka madai ya uwepo wa deni alilokopa benki mwaka 1984 yaliyosababisha mwaka 2003 nyumba aliyoiacha kuuzwa kwa njia ya mnada ambao ulilalamikiwa kugubikwa na utata.
#BMGHabari
Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Manispaa ya Ilemela, Shukrani Kyando (kushoto) akikabidhi hati hiyo kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (kulia) kwa ajili ya kumkabidhi mjane Prucheria Balilemwa (hayuko pichani).
Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (kulia) akimkabidhi mjane Prucheria Balilemwa haki ya nyumba yake iliyokuwa imeuzwa kiutata.
Bibi Prucheria Balilemwa akionyesha hati ya nyumba yake baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (wa pili kulia). Kulia ni Mkuu wa Wilaya Ilemela Dkt. Severine Lalila aliyeshuhudia pia makabidhiano hayo.
Bibi Prucheria Balilemwa ambaye kwa sasa anasumbuliwa na maradhi ya kupooza amemshukru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumsaidia kupata haki yake.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.