LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Misungwi akabidhi bajaji kwa mama mwenye ulemavu "Serikali inawathamini"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Juma Sweda amewataka wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kutokana na mapato ya ndani kuirejesha kwa wakati ili kuwanufaisha walengwa wengine.

Sweda alitoa kauli hiyo wakati akimkabidhi pikipiki ya magurudumu matatu (bajaji) mkazi wa Nyang’homango wilayani humo, Eunice Joshua ambaye ana ulemavu wa viungo.

Eunice alinunua pikipiki hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni saba baada ya kupata mkopo kutoka Halmashauri ya Misungwi ambapo alimshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kuhakikisha walemavu, wanawake na vijana wananufaika na mikopo hiyo ya Halmashauri.

"Walemavu katika jamii yetu hawako wengi, hivyo kuwapata wote 10 wajiunge kwenye kikundi kikundi kimoja ili uwakopeshe ni ngumu hivyo tumevunja huo utamaduni na kumkopesha peke yake" alisema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi Kisena Mabuba.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.