LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella akutana na Watendaji Nyamagana, Ilemela

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) amekutana na watendaji wa Mitaa na Kata kutoka Halmashauri za Jiji la Mwanza (Nyamagana) na Manispaa ya Ilemela na kuwataka kusimamia vyema zoezi la kubaini majengo yanayopaswa kuingia kwenye mfumo wa kulipiwa kodi ya majengo.

Aidha Mongella amewataka viongozi hao kushiriki vyema kwenye kuhamasisha wananchi kulipa kwa wakati kodi ya viwanja, majengo pamoja na zoezi la utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo ambavyo awamu hii vimeboreshwa zaidi.

Mongella aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji hao kilichofanyika Jumanne Februari 16, 2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikiwa ni mwendelezo wake wa kukutana na makundi mbalimbali ambapo tayari amekutana na wafanyabiashara wadogo.
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Emmanuel Tutuba (kushoto) akizungumza kwenye kikao hicho. Katikati ni Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela John Wanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba akifafanua jambo kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga akizungumza kwenye kikao hicho.
Watendaji na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.