LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mfanyabiashara Tarime apandishwa kizimbani kwa mara ya tano

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com 
Na Helena Magabe, Tarime
Kesi ya tuhuma za mauji inayomkabiri mfanyabiashara katika wilaya Tarime mkoani Mara, Lucas Sotel imepigwa tarehe tena kwa mara ya tano na Mtuhumiwa kurudishwa rumande.

Mfanyabiashara huyo anatuhumiwa kumsababishia kifo kijana Wankuru Nyamuhanga mkazi wa Kijiji cha Buriba wilayani Tarime Agosti 09, 2014.

Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi, Issa Bukuru amememwambia Hakimu Mkazi Wilaya Tarime kuwa faili la kesi hiyo bado liko ofisi ya mashitaka hivyo upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Mkazi Charles Mzava amesema kesi hiyo itatajwa tena March 30,2021.

No comments:

Powered by Blogger.