LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mlizoea kwenda Dodoma kupanga bajeti, hilo halipo tena- RC Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amewataka viongozi wa wilaya na watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanawajibika ipasavyo ili kukamilisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/22 kwa kujumuisha vipaumbele vyote muhimu.

Mongella aliyasema hayo Machi 10, 2021 wakati akifungua kikao cha kujengeana uelewa wa pamoja baina ya viongozi na watendaji kutoka idara mbalimbali mkoani Mwanza kuhusu mapendekezo ya bajeti hiyo.

Aidha Mongella alisisitiza kuwa viongozi kutoka ofisi za wakuu wa wilaya pamoja na watendaji kutoka ofisi za wakurugenzi wa halmashauri wanapaswa kuhakikisha wanasimamia vyema ukamilishaji wa mapendekezo hayo wakiwa kwenye ofisi zao badala ya kufikiria ule utaratibu wa kizamani wa watendaji kukutana Dodoma kukamilisha kazi hiyo.

Katika kikao hicho halmashauri mkoani Mwanza ziliwasilisha mapendekezo yake ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/22 na kujadiliwa kwa ajili ya kufanyiwa maboresho kabla ya kuwasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.
#BMGHabari
Wakuu wa Wilaya mkoani Mwanza wakifuatilia kikao hicho.
Wakuu wa Wilaya za Mkoa Mwanza wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wa kikao hicho wakiteta jambo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.