LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Shinyanga awapa heko vijana walioanzisha kiwanda cha Chaki

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa amebeba maboksi ya chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia chaki muda mfupi baada ya chaki hizo kutolewa katika mitambo ya uzalishaji katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga leo Jumanne Machi 2,2021. Katikati ni Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa, kulia ni Mhandisi mkuu wa kiwanda hicho Amani Daniel.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia namna uzalishaji wa chaki unavyofanyika katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia namna uzalishaji wa chaki unavyofanyika kwenye Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia chaki zilizoanikwa juani muda mfupi baada ya chaki hizo kutolewa katika mitambo ya uzalishaji katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akizungumza katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) changamoto wanazokutana nazo wakati wa uzalishaji wa chaki ikiwa ni pamoja na kukosa masoko
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa pili kushoto) akizungumza katika Stoo ya kuhifadhia chaki kwenye Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) kulia ni Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa, kushoto ni Mhandisi mkuu wa kiwanda hicho Amani Daniel wakiwa wameshikilia maboksi ya chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) na viongozi mbalimbali wakiwa wameshikilia maboksi ya chaki.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 Blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ametembelea Kiwanda cha Kutengeneza Chaki cha ‘Shinyanga Standard Chalk’ kilichopo Mjini Shinyanga na kujionea jinsi uzalishaji wa chaki unavyofanyika na kutoa agizo kwa Wakuu wa Shule katika wilaya hiyo kununua chaki hizo.

Mboneko amefanya ziara katika kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga Jumatatu Machi 2,2021.

Akizungumza kiwandani hapo, Mboneko amewapongeza vijana walioanzisha kiwanda hicho kwa kutengeneza chaki mzuri na bora na kutoa agizo kwa Wakuu wa shule zilizopo katika wilaya ya Shinyanga na kuahidi kutafuta masoko zaidi kwenye wilaya zingine.

“Natoa agizo kwa wakuu wa shule zote watumie chaki zinazozalishwa katika kiwanda chetu cha Shinyanga, kuna chaki za kutosha nataka chaki hizi zinunuliwe. Hatuwezi kununua chaki nje ya Shinyanga wakati tunazo hapa kwetu kwenye kiwanda chetu,tena ni chaki nzuri sana na wazalishaji wanafuata taratibu zote za uzalishaji”,amesema Mboneko.

“Nataka kila shule inunue Boksi moja hadi mawili. Mzigo upo wa kutosha na vijana hawa wapo tayari kuwasambazia chaki hadi kwenye shule zenu”,ameongeza Mboneko.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana walioanzisha Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa Hashim amesema walianza uzalishaji wa chaki mwezi Aprili 2020 na sasa wana uwezo wa kuzalisha katoni 102 kwa siku.

Amesema licha ya uzalishaji mkubwa wanaofanya bado changamoto kubwa ni ukosefu wa masoko kutokana na soko la ndani kusuasua akibainisha kuwa endapo soko la ndani likiwa zuri basi wataweza kuuza chaki hizo nje ya wilaya ya Shinyanga ambapo amemshukuru Mkuu wa wilaya hiyo, Jasinta Mboneko kuwaunga mkono kwa kuhamasisha wakuu wa shule kununua chaki katika kiwanda hicho.

No comments:

Powered by Blogger.