LIVE STREAM ADS

Header Ads

Geita watakiwa kuendeleza mapambano dhidi ya Malaria

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Watoa huduma za afya kwa kushirikiana na jamii mkoani Geita wametakiwa kuendeleza jitihada za kupambana na Malaria, baada ya mradi wa kudhibiti ugonjwa huo uliokuwa unatekelezwa na Chama cha Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania (APHFTA) kufikia tamati.

Mkurugenzi Mtendaji wa APHFTA, Dkt. Samwel Ogillo alitoa rai hiyo wakati wa kikao cha kuhitimisha mradi huo kilichowashirikisha wadau mbalimbali wa afya kutoka Wilaya za Mkoa Geita.

Dkt. Ogilo alisema kupitia mradi huo, maabara mbalimbali zimeboreshwa, watoa huduma za afya wamejengewa uwezo wa kutoa huduma bora za kuzuia na kutibu Malaria pamoja na kuwaelimisha wanafunzi mashuleni ili kutambua namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

Akifungua kikao hicho, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Geita, Arnold Msuya alisisitiza kuwa watumishi na watendaji mbalimbali wa Serikali mkoani humo watahakikisha wanaendeleza jitihada zilizokuwa zinafanywa na APHFTA katika kudhibiti Malaria hata baada ya mradi kufikia tamati huku akiwahimiza watoa huduma za afya kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kupitia mradi huo.

Baadhi ya watoa huduma za afya mkoani Geita wakiwemo wenye maduka ya kuuza dawa walitoa shukurani kwa APHFTA kwa kuwajengea uwezo wa kupitia mafunzo mbalimbali pamoja na mikopo iliyowasaidia kuboresha huduma zao hususani katika kupambana na Malaria.

Katika kipindi cha mwaka 2017/21 taasisi ya APHFTA kwa ufadhili wa wadau wa maendeleo kutoka uingereza (Comic Relief na GSK) ilikuwa ikitekeleza mradi wa kupambana na Malaria mkoani Geita hatua iliyosaidia kushusha kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 38.1 mwaka 2015/16 hadi asilimia 17 mwaka 2017/18.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji wa APHFTA, Dkt. Samwel Ogillo akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa Geita, Arnold Msuya akifungua kikao hicho ambapo alisisitiza watoa huduma za afya mkoani humo kuendeleza jitihada za kupambana na Malaria hata baada ya mradi uliokuwa unatekelezwa na APHFTA kufikia ukomo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho.
Mwenyekiti wa APHFTA Kanda ya Ziwa, Dkt. Felician Ndauzi alisema mradi wa kupambana na Malaria mkoani Geita uliwasaidia watoa huduma binafsi za afya mkoani humo kuboresha huduma zao.
Wadau wa afya mkoani Geita wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.