LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge wa Butiama aguswa na wanafunzi wanaoteswa na lifti barabarani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Ujenzi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kirumi unaofanywa na wananchi kwa kushirikiana na juhudi za mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini utaongeza ufaulu na kupunguza mimba kwa wanafunzi wanaopata vishawishi watembeapo umbali wa takribani kilomita 18 hadi kufika Shule ya Sekondari Mmazami Kata ya Bukabwa Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kirumi, Mitagato Damiana na kuoneza kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakiacha Shule huku takwimu za ufaulu zikiwa zinashuka kutokana na kutembea kwa mguu kutoka Kirumi hadi Shule ya Sekondari ya Mmazami ambapo wanafunzi wanalazimika kuamka saa 11 alajii na kupanga foleni barabara ya Tarime-Mwanza wakisubiria lifti kutoka kwa wasamalia wema na kujikuta wakiangukia kwenye vishawishi.

"Tunajua kuwa moja kati kipaumbele cha mbunge wetu Jumanne Sagini ni elimu na sote ni mashuhuda kwenye sekta hiyo anazidi kufanya vizuri Butiama, hivyo ametoa ushirikiano wa kutosha katika ujenzi wa Shule hii, mbali na ahadi anazoendelea kuzitoa kwetu ameleta mabati 72 na mifuko 20 ya saruji ambapo alitupa hamasa ya kuamka na kushiriki ujenzi kwani muda mrefu tulikuwa hatujapata mtu wa kutushika mkono" alisema Damiana.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Kirumi, Charles Andrew alisema Shule hiyo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi tangu mwaka 2014 baada ya kuona watoto wao wanatembea umbali mrefu kwenda Shule ya Mmazami na baadhi yao walikuwa hawafiki shuleni kwa wakati na hivyo kuacha Shule kutokana na adhabu za mara kwa mara za uchelewaji walizokuwa wakipewa.

Nao baadhi ya wanafunzi walimshukuru mbunge wa Buiama kwa juhudi zake na kueeleza kuwa huwa wanajipanga barabarani kusubiria lifti za magari ya abiria au mizigo yanayooka Sirari, Tarime na nchi jirani ya Kenya ambapo wanafunzi wachache wanabebwa na wengine wanaachwa.

"Muda mwingine inaweza kuja pikipiki au gari ndogo inachagua mtu wa kupanda hasa wasichana ndio wanapata nafasi hizo chache ambazo zinavishawishi vingi" walisema wanafunzi hao.
Mwonekano wa majeno ya Shule ya Sekondari Kirumba inayojengwa ili kuondoa adha ya wanaunzi kutembelea umali mrefu kwenda Shule ya Sekondari Mmazami kusaka elimu.
Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Butiama unaendelea vyema na wadau wanahimizwa kutoa ushirikiano ili kukamilika kwa wakati.
Baadhi ya viongozi wilayani uiama wakiwa kwenye ukauzi wa majengo ya Shule mpya ya Kirumi.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.