LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kigogo wa Bandari adakwa baada ya kusakwa na TAKUKURU

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza imemkamata aliyekuwa Mhasibu wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Mkoa wa Kigoma, Madaraka Robert ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Frank Mkilanya amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 19, 2021 na kwamba anakabiliwa na tuhuma za rushwa, uhujumu uchumi na ukwepaji kodi kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 153.5.

Mkilanya aliyasema hayo Aprili 20, 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza na kuongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa mafichoni katika eneo la Nyasaka Manispaa ya Ilemela baada ya kutafutwa na taasisi hiyo tangu Agosti 2020.

Aidha Mkilanya alibainisha kwamba mtuhumiwa huyo anatarajiwa kuunganishwa na watuhumiwa wengine watano ambao wako mbaroni kutokana na tuhuma hizo.
Na Michael Jamson, Mwanza
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Frank Mkilanya, akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, alipotoa taarifa ya utendaji kazi.
Viongozi mbalimbali wa TAKUKURU mkoani Mwanza wakifuatilia taarifa hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.