LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Mwanza awakumbuka wenye uhitaji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Mwanza, Nyiriza Makongoro kwa kushirikiana na Kamata ya Utekelezaji amesherehekea Sikukuu ya Eid El Fitr mwaka huu 2021 kwa kutoa msaada wa bidhaa mbalimbali kwa makundi ya watu wenye uhitaji katika Kata ya Butimba wilayani Nyamagana.

 Makongoro ameyataja makundi yaliyonufaika na msaada wa bidhaa hizo ikiwemo sukari kilo 50, mafuta ya kupitia lita 20, mchele kilo 50 na sabuni katoni 25 ni watoto yatima, wazee pamoja na wenye ulemavu ambapo hafla hiyo imefanyika katika ofisi za CCM Kata ya Butimba.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Mwanza, Nyiriza Makongoro.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mahitaji yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Mwanza, Nyiriza Makongoro yameacha alama ya upendo katika mioyo ya watu wenye uhitaji.
Viongozi mbalimbali wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Mwanza, Nyiriza Makongoro (wa tatu kulia).
Makundi mbalimbali ya watu wenye uhitaji katika Kata ya Butimba waliofika kwa ajili ya kupata msaada wa bidhaa kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Mwanza, Nyiriza Makongoro ikiwa ni sehemu ya kusherehea Sikukuu ya Eid El Fitr 2021.
Makundi mbalimbali ya watu wenye uhitaji katika Kata ya Butimba waliofika kwa ajili ya kupata msaada huo.

No comments:

Powered by Blogger.