LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wachimbaji wadogo Masasi waneemeka na mafunzo kutoka GST

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Timu ya wataalamu wa utafiti,uchenjuaji na uchunguzi wa madini kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) wamefika mkoani Mtwara kwa ajili ya kuwapa mafunzo wachimbaji wadogo wa madini juu ya namna bora ya uchukuaji sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa madini.
Na Idara ya Habari Maelezo
Mjiolojia Zortosy Mpangile akionesha namna ya uchukuaji wa sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa madini wakati alipokuwa akiwafundisha kwa vitendo wachimbaji wadogo wa madini katika Machimbo ya Chipite wilayani Masasi, Mkoani Mtwara ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa mafunzo ya namna bora ya uchukuaji sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa madini yanayotolewa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).
Mhandisi Uchenjuaji Lilian Anton kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa madini Tanzania GST akiwaonesha wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya Chipite Wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara, namna bora ya uchotaji udongo/sampuli kwa ajili ya kupeleka Maabara ili ukafanyiwe uchunguzi wa Madini.
Mjiolojia Raymond Pius akichanganya udongo kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo kwa Wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya Chipite Wilayani Masasi, mkoani Mtwara juu ya namna bora ya uchukuaji sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa madini yanayotolewa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).
Picha ya Pamoja baina ya wachimbaji wadogo wa Madini katika Machimbo ya Chipite Wilayani Masasi, Mkoani Mtwara na wataalamu wa Utafiti na Uchenjuaji wa Madini kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa madini Tanzania GST walipotembelea machimbo hayo kwa ajili ya kutoa elimu kwa Vitendo juu ya namna bora ya uchukuaji sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa madini.

No comments:

Powered by Blogger.