BITEKO atoa miezi miwili, mgodi wa MMG mkoani Mara
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa muda wa miezi miwili kwa uongozi mpya wa mgodi wa dhahabu wa MMG ulipo Wilaya Musoma mkoani Mara kuhakikisha unalipa deni la zaidi ya shilingi 30 kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Seka ulipo mgodi huo.
Waziri Biteko ametoa agizo hilo Julai 19, 2021 alipotembelea mgodi huo kufuatilia utekelezaji wa masuala mbalimbali ambayo hapo awali yalikuwa yakilalamikiwa ambapo ameridhishwa na hatua zilizochukuliwa katika kuyashughulikia.
Amesema awali mgodi huo ulikuwa na matatizo makubwa lakini katika kipindi kifupi cha uongozi mpya kumekuwa na mabadiliko ikiwemo kuondoa malalamiko ya kutowalipa wafanyakazi, kutolipa ushuru na tozo mbalimbali za Halmashauri.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mgodi wa GGM, Yury Chernomorchenko ameridhia kutelekeza kwa wakati agizo la Waziri Biteko kwa kusaini makubaliano na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Musoma ya kulipa deni hilo huku akibainisha kuwa tayari mgodi huo umeanza kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo kijijini hapo.
Awali Diwani wa Kata ya Nyamrandirira, Nyeoja Wanjara alisema uongozi uliopita wa mgodi huo uliacha deni la shilingi milioni 36 na kuomba Waziri Biteko kuingilia kati ili lilipwe lakini pia kuhimiza mgodi kuendelea kusaidia miradi inayoanzishwa na wananchi ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na ukarabati wa barabara.
Waziri Biteko alihitimisha ziara yake kwa kutembelea mgodi wa ‘CATA Mining’ ulipo Kiabakari wilayani Butiama na kuelekeza uongozi wa mgodi huo kutekeleza shughuli zake kwa mujibu wa sheria hususani katika utoaji wa tenda mbalimbali.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa mgodi wa MMG, Yury Chernomorchenkoakieleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mgodi huo baada ya kufanyika mabadiliko ya kiuongozi.
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akisalimiana Mkuu wa Mkoa Mara, Ally Hapi (kulia) alipowasili ofisini kwake kabla ya kuanza zira ya kutembelea migodi ya MMG na CATA Mining iliyopo mkoani humo.
Waziri wa Mdini, Doto Biteko (kushoto) akisalimiana na Diwani wa Kata ya Nyamrandirira, Nyeoja Wanjara (katikati) alipowasili katika mgodi wa dhahabu MMG uliopo wilayani Musoma. Kulia ni Mkurugenzi wa mgodi huo Yury Chernomorchenko.Mkurugenzi wa mgodi wa MMG, Yury Chernomorchenkoakieleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mgodi huo baada ya kufanyika mabadiliko ya kiuongozi.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika mgodi wa MMG wilayani Musoma.
Sehemu ya mwonekano wa bwawa la kuhifadhia tope sumu (TFS) katika mgodi wa MMG. Waziri Biteko ameagiza ujenzi wa bwawa jipya ukamilike kwa wakati katika mgodi huo kwani lililopo halikidhi mahitaji.
Sehemu ya mwonekano wa machimbo (PIT) mapya katika mgodi wa MMG.
Viongozi wa mgodi wa MMG pamoja na Halmashauri ya Wilaya Musoma wakisaini makubaliano kwa ajili ya mgodi huo kulipa deni la shilingi milioni 36 ndani ya miezi miwili kama alivyoagiza Waziri Biteko kwa Serikali ya Kijiji cha Seka ulipo mgodi huo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) alitembelea pia mgodi wa 'CATA Mining' uliopo Kiabakari wilayani Butiama na kuridhishwa na maendeleo ya mgodi huo huku akiagiza shughuli zote kufanyika kwa kuzingatia sheria ikiwemo taratibu za utoaji tenda kutangazwa kwa uwazi ili kutoa fursa kwa wazawa pia kushiriki shughuli hizo.
Sehemu ya mwonekano wa PIT katika mgodi wa 'CATA Mining' wilayani Butiama.
Mwonekano wa kinu cha kuchenjulia madini katika mgodi wa 'CATA Mining' wilayani Musoma unaomilikiwa kwa ubia na JWTZ (wenye eneo) na mwekezaji kutoka Canada.
Tangu kufanyika kwa mabadiliko ya sheria na kanuni za usimamizi madini, Mkoa Mara umechangia ongezeko la makusanyo ya Serikali hadi kufikia shilingi bilioni 109 mwaka 2020/21 kutoka shilingi bilioni 32 mwaka 2015/16 huku madini ambayo tayari yameuzwa katika soko la madini mkoani humo yakifikia tani 3.3 yakiwa na thamani ya shilingi bilioni 360 ambapo kati ya hizo, mrabaha ulioingia serikalini ni shilingi bilioni 26.

Tazama BMG TV hapa chini
No comments: