LIVE STREAM ADS

Header Ads

Makondakta jijini Mwanza wakabidhi msaada Shule ya Msingi Sahara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Umoja wa Makondakta na Wasaidizi Wake jijini Mwanza umeunga mkono jitihada za ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Sahara kwa kukabidhi mifuko sita ya seruji pamoja na vifaa mbalimbali vya usafi.

Mwenyekiti wa umoja huo, Murimi Juma amesema mifuko hiyo pamoja na vifaa vya usafi ikiwemo diaba pamoja na ndoo itasaidia kuibua ari ya wadau wengine kujitokeza ili kusaidia ukamilishaji wa maboba shuleni hapo.

Amesema mara kwa mara umoja huo kupitia michango ya wanachama wake umekuwa mstari wa mbele kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuhimiza masuala ya usafi na usalama katika vituo vya kazi.

Aidha ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha janga la Corona, umoja huo unahakikisha katika unaweza ndoo zenye maji tiririka pamoja na sabuni kwa ajili ya abiria kunawa mikono kabla ya kupanda ama kushuka kwenye daladala.

Naye Mwalimu wa Mzingira na Miundombinu Shule ya Msingi Sahara, Mwl. Arubugast Nyalinga amesema jitihada za umoja huo kushiriki kwenye shughuli za maendeleo katika jamii ni za kuigwa na wadau wengine akibainisha kuwa hiyo ni mara ya pili umoja huo unatoa msaada shuleni hapo.

“Tunashukuru Umoja wa Makondakta na Wasaidizi Wake kwa kutusaidia simenti za kukamilisha ujenzi wa madarasa” amesema mwanafunzi wa Shule hiyo, Sada Ramadhan huku mwanafunzi Dianke Ally akiongeza kuwa ndoo na diaba hizo zitawasaidia kufanya usafi madarasani na kwenye vyoo.

Katika hatua nyingine umoja huo umefanya usafi katika mitaa mbalimbali jijini Mwanza ikiwa ni utaratibu wake wa kufanya hivyo kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuunga mkono kwa vitendo kauli iliyotolewa na aliyekuwa Makamu wa Rais ambaye sasa ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Umoja wa Makondakta na Wasaidizi Wake jijini Mwanza, Murimi Juma (wa pili kushoto) akikabidhi mifuko ya saruji kwa uongozi wa Shule ya Msingi Sahara.
Mwenyekiti wa Umoja wa Makondakta na Wasaidizi Wake jijini Mwanza, Murimi Juma (wa pili kushoto) akikabidhi diaba kwa ajili ya usafi katika Shule ya Msingi Sahara.
Mwenyekiti wa Umoja wa Makondakta na Wasaidizi Wake jijini Mwanza, Murimi Juma (wa pili kushoto) akikabidhi ndoo shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Makondakta na Wasaidizi Wake jijini Mwanza, Murimi Juma.
Mwalimu wa Mzingira na Miundombinu Shule ya Msingi Sahara, Mwl. Arubugast Nyalinga.
Mwanafunzi Shule ya Msingi Sahara, Sada Ramadhan akitoa shukurani kwa Umoja wa Makondakta na Wasaidizi Wake jijini Mwanza baada ya kutoa msaada huo.
Mwanafunzi Shule ya Msingi Sahara, Dianke Ally akieleza msaada huo utakavyowasaidia.
Wanachama wa Umoja wa Makondakta na Wasaidizi Wake jijini Mwanza wamefanya usafi katika Vituo mbalimbali vya daladala ikiwemo Stendi ya Igombe, Kemondo, Makoroboi, Dampo pamoja na Natta.
Usafi katika stendi ya Igombe jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Umoja wa Makondakta na Wasaidizi Wake jijini Mwanza, Murimi Juma akiwa na wanachama wa umoja huo kufanya usafi katika mitaa mbalimbali.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.