LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi kulipwa fidia ujenzi wa SGR Mwanza-Isaka

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel amewahakikisha wananchi ambao maeneo yao yatapitiwa na mradi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tano kutoka Fela Mwanza hadi Isaka Shinyanga kuwa watalipwa fidia kwa mjibu wa Sheria.

Aidha ameongeza kuwa mradi huo utatoa fursa nyingi za kiuchumi kwa wananchi ikiwemo ajira zaidi ya elfu kumi pamoja na zabuni za utoaji huduma na usambazaji bidhaa mbalimbali kama vyakula pamoja na usafiri/ usafirishaji.

Mhandisi Gabriel ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni ya kuwajengea uelewa wananchi kuhusu utekelezaji wa mradi wa SGR kutoka Fela hadi Isaka ambayo imeanza Julai 06, 2021 ambapo amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuwasikiliza wataalamu kutoka Shirika la Reli nchini (TRC) watakapopita katika maeneo yao.

Juni 14, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo wenye urefu wa kilomita 341 ambao hadi kukakilika utagharimu takribani shilingi tirioni tatu fedha za Serikali.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.