LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Makilagi azindua Maadhimisho ya Miaka 50 ya Bugando

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi Agosti 06, 2021 akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Robert Gabriel amezindua Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa Hospitali ya Kanda Bugando ambapo shughuli mbalimbali ikiwemo michezo na utoaji huduma za afya zinatarajiwa kufanyika kuelekea kilele cha Maadhimisho hayo Novemba 03, 2021.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi akizungumza kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa Hospitali ya Kanda Bugando ambapo amewahimiza wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono jitihada za ujenzi wa jengo la Saratani katika Hospitali hiyo.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mwanza, Renatus Nkwande ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Bugando amesema maadhimisho hayo ya miaka 50 yanapaswa kusaidia kufanya tafakari ya kina kuhusu Hospitali hiyo ilipotoka, ilipo na inapoelekea ili kusaidia kutoa huduma bora za afya.
Wananchi na wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wafuatilia ufunguzi huo.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita, Flavian Kassala ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) linalomiliki Hospitali ya Bugando amesema uwepo wa Hospitali hiyo ni mkono mwingine wa uinjilishaji unaowagusa watu wote katika kuonja upendo wa Mungu nyakati za furaha na tabu.
Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Kanda Bugando, Dkt. Fabian Massaga amesema Hospitali hiyo imepiga hatua katika huduma za kibingwa tangu kuanzishwa kwake miaka 50 iliyopita ambapo inahudumia wagonjwa wa nje laki 3.5 kwa mwaka na wagonjwa wa ndani elfu 30 kwa mwaka.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Hospitali ya Bugando, Profesa William Mahalu (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi vipeperushi vyenye jumbe mbalimbali kuhusiana na Maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Hospitali ya Bugando, Profesa William Mahalu (kushoto) akimkabidhi Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mwanza Renatus Nkwande vipeperushi vyenye jumbe mbalimbali kuhusiana na Maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Hospitali ya Bugando, Profesa William Mahalu (kushoto) akimkabidhi Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Geita, Flavian Kassala (wa tatu kulia) vipeperushi vyenye jumbe mbalimbali kuhusiana na Maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Hospitali ya Bugando, Profesa William Mahalu (kushoto) akimkabidhi Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine vipeperushi vyenye jumbe mbalimbali kuhusiana na Maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Hospitali ya Bugando, Profesa William Mahalu (kulia) akiteta jambo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga (kushoto).
Mstahiki Meya Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mstahiki Meya Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga wakifuatilia hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali akiwemo Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Renatus Nkwande (kushoto) wakifuatilia ufunguzi huo.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amina Makilagi wakiwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho hayo.
Viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Meya Jiji la Mwanza, Rodrick Ngowi wakifuatilia ufunguzi huo.
Viongozi mbalimbali meza kuu wakifuatilia ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa Hospitali ya Kanda Bugando.
Wajumbe wa Kamati ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa shughuli mbalimbali ikiwemo utoaji huduma za afya na michezo katika kuelekea Novemba 03, 2021 kwenye kilele cha Miaka 50 tangu kuanzishwa Hospitali ya Bugando.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Hospitali ya Kanda Bugando.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi (wa tano kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Viongozi mbalimbali, wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Kanisa Katoliki.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi (wa tatu) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi (wa tatu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wajumbe ya Kamati ya Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa Hospitali ya Kanda Bugando.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi (katikati) akishukuru kwa mapokezi wakati wa uzinduzi wa Miaka 50 ya Hospitali ya Kanda Bugando.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi (wa tatu kulia) akiagana na viongozi mbalimbali wa Kanisa Katoliki baada ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa Hospitali ya Kanda Bugando.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.