LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maandalizi Rock City Marathon yanoga, Unilever watoa Milioni 20

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kampuni ya Unilever Tanzania imekabidhi hundi yenye thamani Tsh. Milioni 20 kwa waandaaji wa mbio za Rock City Marathon ikiwa ni udhamini wa kampuni hiyo katika mbio za Kilomita 2.5 mahususi kwa ajili ya watoto.

Hatua hiyo inatajwa kuwa ni muendelezo wa mkakati wa kampuni hiyo katika kushirikiana na Jamii na Serikali kwa ujumla katika kuhamasisha michezo nchini ili kuibua vipaji, kujenga afya pamoja na kukuza sekta ya michezo nchini.

Mbio za Rock City Marathon zinatarajiwa kufanyika Oktoba 24, 2021 katika viunga vya Rock City Mall jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.