LIVE STREAM ADS

Header Ads

Madiwani wa Arusha wakoshwa na miradi ya kimkakati Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wamefika katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza kujifunza utekelezaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Soko Kuu Mwanza pamoja na Stendi ya Mabasi Nyegezi ambapo wamefurahishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.

Pia madiwani hao wametembelea mradi wa kiwanda cha kufyatua matofali Buhongwa pamoja na vivutio mbalimbali vya utalii jijini Mwanza ikiwemo jiwe la Bismarck eneo la Kamanga pamoja na Kisiwa cha Saanane.

Mstahiki Meya Jiji la Arusha, Maximillian Iranqhe alisema ziara hiyo ya kujifunza utekelezaji wa miradi ya maendeleo na usafi wa mazingira jijini Mwanza itawasaidia kubuni miradi mbalimbali watakaporejea Arusha.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine alisema ziara hiyo ni mwanzo wa ushirikiano baina ya Halmashauri yake na Jiji la Arusha ambapo kupitia ziara mbalimbali za kimafunzo, wataweza kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na namna bora ya kuwapanga wafanyabiashara wadogo katika maeneo rasmi kwani majiji hayo yanafanana.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Maximillian Iranqhe (kulia) akieleza umuhimu wa ziara ya madiwani wake jijini Mwanza. Kushoto ni Mstahiki Meya Jiji la Mwanza, Sima Costantine.
Mstahiki Meya Jiji la Mwanza, Sima Costantine akiteta jambo wakati wa ziara ya madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kutembelea miradi ya maendeleo jijini Mwanza.
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wakitembelea mradi wa stendi ya kisasa Nyegezi inayojengwa na Halmashauri ya jiji la Mwanza kwa zaidi ya shilingi bilioni 14.
Naibu Meya Jiji la Mwanza, Rodrick Nyoye (kushoto) akiwa na madiwani wa Jiji la Arusha walipotembelea kiwanda cha kufyatua matofali jijini Mwanza.
Madiwani wa Jiji la Arusha pia walitembelea ujenzi wa Soko Kuu jijini Mwanza.
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wakiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeji wao Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza walipotembelea eneo la Bismack Rock.

No comments:

Powered by Blogger.